Pamoja
na hayo, Woodward amesema kwamba haitaiathiri k;abu hiyo katika solo la
usajili. "Kutokana na mikataba ya Televisheni, tunakadiria tutakosa
Pauni Milioni 30 za michuano ya Ulaya. Matarajio ya klabu yalikuwa ni
kurejea kwenye Ligi ya Mabingwa naa utaona kwenye usajili wetu,".
![Talks: United legend Ryan Giggs was pictured in Holland for a meeting with Van Gaal on Wednesday](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/05/14/article-2628269-1DD76ACE00000578-317_634x420.jpg)
Mazungumzo: Giwji wa United, Ryan Giggs alipigwa picha nchini Uholanzi akiwa na kikao na Van Gaal Jumatano
Akizungumza
katika mkutano wa simu, alisema: "Katika msimu wa 2013-14, tumemaliza
vibaya katika nafasi ya saba, ambayo inamaanisha hatutashiriki michuano
ya Ulaya.
"Kuwa
na uhakika kila mmoja katika klabu anapambana kuhakikisha msimu ujao
tunakuwa katika kiwango cha juu cha Manchester United.
"Tumefanya
mabadiliko ya bench la Ufundi Aprili, tumefurahi kuwa na Ryan Giggs kwa
kumalizia msimu vizuri. Kwa sasa tunaelekeza nguvu zetu katika kupata
kocha mpya na tarajia atatangazwa muda si mrefu,".
Louis
van Gaal ndiye kocha anayetarajiwa kuichukua Manchester United baada ya
Fainali za Kombe la Dunia atakapoiongoza kwa mara ya mwisho Uholanzi.
Jumatano Giggs alitua Uholanzi na akapigwa picha na inasemakana alikwenda kufanya mazungumzo na Van Gaal kwa niaba ya klabu.
No comments:
Post a Comment