Miaka tisa, Kombe moja: Kocha wa Arsenal, Mfaransa Arsene Wenger alilazimika kubadilisha shati lake baada ya alilokuwa amevaa kuloana bia alizomwagiwa na wachezaji wake wakati wa kushangilia ushindi wa 3-2 uliowapa Kombe la FA jana Uwanja wa Wembley, taji la kwanza kwa klabu hiyo na mocha huyo kwa ujumla baada ya miaka tisa.

Juu juu: Wenger akiwa amebebwa juu juu na wachezaji wake jana

Anaogeshwa mbege: Wenger akimwagiwa bia na wachezaji wake

Aogeshwe huyoo: Wenger akiwa amebebwa na kumwagiwa bia na wachezaji wake.


Serge Gnabry na Alex Oxlade-Chamberlain, kushoto na Santi Cazorla na Nacho Monreal wakiwa wamepozi na Kombe la FA chumba cha kubadilishia nguo Uwanja wa Wembley jana

Kutoka kushoto ni Santi Carzorla, Mesut Ozil, Per Mertesacker, Serge Gnabry, Lukas Podolski na Aaron Ramsey

Podolski akishangilia mbele ya mashabiki

Mmoja wa mashabiki wa Arsenal akiwa kifua wazi kushangilia ubingwa
No comments:
Post a Comment