PONDA ARUDISHWA TENA RUMANDE.
Kiongozi wa Taasisi ya Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda
ameendelea kusota rumande baada ya kesi yake kuahirishwa kwa mara
nyingine kwa kuwa jalada la kesi yake, halijarudi kutoka Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam lilikoitishwa kwa ajili ya mapitio.Kesi hiyo iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa
wa Morogoro mwaka jana, iko mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo,
Mary Moyo na imekuwa ikitajwa kwa zaidi ya miezi sita, huku Sheikh Ponda
akiendelea kusota rumande baada ya kunyimwa dhamana.
No comments:
Post a Comment