HIZI ndizo mpya za msimu ujao za Manchester United?
Jezi
mpya za Mashetani Wekundu zimevuja kwenye mitandao ya kijamii, ambazo
ni za Nike zikiwa na rangi nyekundu na chata la rangi nyeupe wadhamini
wapya, Chevrolet kwa mbele.
Jezi hizo zina zipu nyeusi kutokea shingoni kuelekea chini na ufito mweusi kwenye pindo za mikono na mabegani.
Pamoja
na hayo haijathibishwa kama habari kuhusu jezi hizo ni sahihi. United
ilitangaza Julai mwaka 2012 udhamini wa jezi na Chevrolet, ambao
watakuwa wakilipa Pauni Milioni 25 kwa mwaka kuweka jina lao kwenye jezi
za timu hiyo kuanzia msimu ujao.
Wadhamini wa sasa wa United, Aon, hawataonekana tena kwenye jezi za timu hiyo kuanzia msimu ujao.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England wanaweza kuvuna fedha zaidi kutokana na ongezeko la dau la udhamini wa vifaa vya michezo.
United
imekuwa kwenye mazungumzo na Nike kuingia Mkataba wao mpya wa miaka 13,
lakini kwa mujibu wa Daily Mail, Wekundu hao wanajiandaa kuingia kwenye
miezi mingine sita ya kusaka dili zuri zaidi kabla ya kujitia pingu.
Mkataba wa sasa wa Nike unamalizika mwishoni mwa msimu ujao.
Uwanjani,
United inajaribu kufufua makali yake msimu huu baada ya kipigo ambacho
hawakutarajia kutoka kwa Olympiacos kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
United
iliyofungwa kwenye mechi ya kwanza ya Hatua ya 16 Bora mjini Athens,
Ugiriki inatumai kuzinduka itakaposafiri hadi Uwanja wa The Hawthorns
kesho kumenyana na wenyeji West Bromwich Albion katika mchezo wa Ligi
Kuu.
![This season's model: United's 2013/14 strip](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/03/07/article-2575478-1AEF1B1B00000578-352_306x423.jpg)
![Robin van Persie wears United's away kit this season](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/03/07/article-2575478-1B6F0BD000000578-574_306x423.jpg)
Hawataonekana
tena kuanzia msimu ujao: Jezi za sasa za nyumbani za United iliyovaliwa
na Wayne Rooney (kushoto) na za ugenini iliyovaliwa na Robin van Persie
(kulia)
![All white on the night: United's third kit is this white number](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/03/07/article-2575478-1BBD572B00000578-484_634x430.jpg)
Jezi ya tatu ya United
No comments:
Post a Comment