Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo na tetesi za wanamuziki Drake na Rihanna kwamba wamerudisha mahusiano yao ya kimapenzi.
Ingawa wawili hao waliopachikwa jina la
‘AubRih’ (Kwa maana ya Aubrey na Rihanna) mpaka sasa wamekuwa
wakisisitiza na marafiki lakini vitendo vya hivi karibuni vinaonyesha
kuna kitu zaidi ya urafiki kati yao. Rihanna na amekuwa akionekana na
Drake wakiongozana kwenye ziara ya kimuziki ya Drake barani ulaya.
Mara ya kwanza walionekana pamoja nchini Ufaransa, kisha Ujerumani na jana usiku walionekana pamoja jijini Manchester – England.
Na hizi ni picha za ushahidi wa wawili hao walivyokuwa wakijiachia kwenye mitaa ya jiji la Manchester usiku jana.
No comments:
Post a Comment