MADOGO wanaotikisa katika ulimwengu wa muziki Bongo, Abdulaziz Chende
‘Dogo Janja’ na Asilahi Isihaka ‘Aslay’ wamedaiwa kuvunja uchumba wa
jamaa aliyefahamika kwa jina la Fikiri Chodas na Farida.
Tukio hilo lilitokea usiku wa Machi 7, mwaka huu, Newala mkoani
Mtwara wakati wasanii hao walipokuwa wamekwenda kufanya ziara ya
kimuziki.
Kwa mujibu wa chanzo makini, baada ya madogo hao kufanya shoo kali
mjini humo, Farida aliwang’ang’ania wasanii hao waliokuwa wakijiandaa
kwenda kulala katika hoteli waliyofikia ndipo Fikiri alipokasirika.
Uvumilivu ulimshinda Fikiri, akamvaa Dogo Janja na kumtaka aachane na
mpenzi wake, mchumba wake huyo naye akaja juu na kuhamia kwa Aslay
ndipo vurugu ilipotokea ambapo Fikiri alihangaika kumkwida ili kumuokoa
mpenzi wake asiondoke na wasanii hao.
Kuonesha mwanamke huyo alikuwa ‘amekolea’ kwa wasanii hao, alianza
kumporomoshea mpenzi wake matusi ya nguoni na kudai amuache kwani
‘wametembea’ naye siku moja tu.
Fikiri alipoona mpenzi wake huyo anamkana, aliamua kutangaza kummwaga papo hapo.
Jitihada za mapaparazi wetu kufuatilia sakata hilo kwa undani zilizaa matunda baada ya kufanikiwa kunasa video ya timbwili hilo
Jitihada za mapaparazi wetu kufuatilia sakata hilo kwa undani zilizaa matunda baada ya kufanikiwa kunasa video ya timbwili hilo
Mapaparazi wetu walimtafuta Dogo Janja kwa njia ya simu, alipopatikana alifunguka:
“Kweli siku ile tulipomaliza shoo tu tulimuona huyo demu (Farida)
anakuja kwetu. Ghafla jamaa akatokea na kuanza kugombana. Sisi
tuliondoka sasa kama jamaa kamuacha mpenzi wake ni yeye mwenyewe, sisi
hatukuondoka naye,” alisema Dogo Janja
No comments:
Post a Comment