Kiwango cha Robin van Persie kimekuwa sio cha kuvutia msimu huu akifunga mabao 11 katika mechi 15 za ligi. Maneno yake kwamba wachezaji wenzao wanacheza kwenye maeneo ambayo yeye hupendelea kucheza yamezidi kuweka wasiwasi kwenye hatma yake ndani ya klabu hiyo.
Pia
tetesi za kwamba mazoezi magumu ya Moyes hayamsaidii Van Persie zaidi
kumuongezea majeruhi - huku ikisemekana kwamba van Persie kwamba mbinu
sahihi na bora za mazoezi za kocha Rene Mulensteen ndizo zilizochangia
kiwango kizuri katika msimu wa kwanza wa Van Persie Old Trafford. Baada
ya World Cup, mnamo mwezi August Van Persie atakuwa na miaka 31, muda
ambao mshambuliaji atakuwa akitegemea zaidi namna ya kuji-position na
umaliziaji kuliko kasi.
Jukumu la RVP chini ya utawala David Moyes
Van Persie ni namba 9 na nusu, kama ambavyo anasemaga mwenyewe. Anapenda kurudi nyuma, kuanzisha mashambulizi na kwenda mbele kumalizia mashambulizi. Pia ni mzuri hewani na ndani ya box, ni mshambuliaji fundi na mmoja ya washambuliaji bora duniani. Dhidi ya Olympiakos, alipata nafasi moja nzuri ya kufunga baada ya kupokea krosi kutoka kwa Chris Smalling, lakini akauhamisha mpira upande wa kulia na kutoka nje ya mwamba, lakini unaweza kujiuliza kwanini United wanang'ang'ania kupiga makrosi kwa Rooney na Van Persie - washambuliaji hatari duniani wakati wanweza kumtumia kiungo mchezeshaji kuwapitishia mipira na wenyewe wamalizie.
Jukumu la RVP chini ya utawala David Moyes
Van Persie ni namba 9 na nusu, kama ambavyo anasemaga mwenyewe. Anapenda kurudi nyuma, kuanzisha mashambulizi na kwenda mbele kumalizia mashambulizi. Pia ni mzuri hewani na ndani ya box, ni mshambuliaji fundi na mmoja ya washambuliaji bora duniani. Dhidi ya Olympiakos, alipata nafasi moja nzuri ya kufunga baada ya kupokea krosi kutoka kwa Chris Smalling, lakini akauhamisha mpira upande wa kulia na kutoka nje ya mwamba, lakini unaweza kujiuliza kwanini United wanang'ang'ania kupiga makrosi kwa Rooney na Van Persie - washambuliaji hatari duniani wakati wanweza kumtumia kiungo mchezeshaji kuwapitishia mipira na wenyewe wamalizie.
Kwa
macho tu, ushirikiano wa Rooney na RVP unaonekana kuwa bora kabisa
katika premier league, hata barani ulaya. Lakini tatizo sasa ni kwamba
Van Persie anacheza zaidi kama 9 kuliko navyocheza kama namba 10, ambapo
inapaswa kwamba wakati RVP amerudi nyuma Rooney aende mbele kucheza
nafasi ya RVP, mabadilishano hayo sasa hayafanyiki baina yao, aidha
barani ulaya au kwenye premier league. Kama ambavyo katika picha ya
mchezo wa dhidi ya Olympiakos,. Rooney mara chache sana aliingia ndani
ya box, sababu kubwa haswa ni kutokucheza vizuri kwa mawinga pia huduma
mbovu kutoka kati kati ya kiwanja. Alichokuwa akifanya zaidi kuchukua
mipira iliyokufa kutoka Ashley Young na Antonio Valencia na kujaribu
kumpelekea wachezaji wa mbele.
Kuliko
kucheza mfumo wa 4-4-1-1 huku Rooney akiwa nyuma ya Van Persie, inaweza
kuwa jambo la busara kumchezesha Kagawa au Juan Mata nyuma ya
RVP-Rooney katika mfumo wa Diamond au 4-3-1-2. Hili litapelekea wote
wawili RVP na Rooney kuwavuta mabeki wa kati pembeni, na hivyo
kumuwezesha namba 10 aidha apige shuti kutokea nje ya box au aingie
ndani kupitia mwanya ulioachwa wazi na mabeki wa kati watakaokuwa
wakiwakaba RVP na Rooney.
Akiwa
kwenye fomu RVP ni mmoja ya washambuliaji bora barani ulaya lakini
katika mfumo wa sasa wa David Moyes anakuwa hapewi nafasi ya kutosha ya
kurudi nyuma wala kucheza vizuri na movements zake za kuwakimbia mabeki.
Badala yake anaambiwa acheze ndani ya box na jambo hilo linamlimiti
kucheza katika ubora wake. Kwa mchezaji mkubwa kama RVP, huu mfumo
unamchosha na bila huduma bora kutoka kwa mawinga, ataendelea kucheza
chini ya kiwango.
![rvp3](http://thinkfootball.co.uk/wp-content/uploads/2014/03/rvp3.png)
HITIMISHO
Kwenye
timu ya taifa Robin van Persie anae Arjen Robben ambaye hutokea upande
wa kulia kuingia kati na kupenyeza mipira kati kati ya mabeki wa kati.
Pia yupo Wesley Sneijder ambaye ni master pasi za mwisho kwa karibu na
hata mipira mirefu. Anaweza pia kucheza nyuma ya namba 9 halisi kama
Klaas-Jan Huntelaar, jukumu ambalo analiweza kisawa sawa, kutokana na
ubunifu na ufundi alionao. Kwa Van Persie mchezo sasa wa United lazima
acheze chini ya kiwango, United inabidi wabadilike kucheza bila mawinga
halisi, Mata na Kagawa wanaweza kuchukua mashavu wakicheza kama viungo
washambuliaji wanaoingia ndani - wakimtegemea Rooney kupandisha timu
mbele na pia kuongeza wa wachezaji wa United katikati - eneo ambalo
United wamekuwa dhaifu kwa misimu kadhaa sasa.
No comments:
Post a Comment