MSHAMBULIAJI
Robin van Persie amepuuza tetesi kwamba atahama Manchester United
mwishoni mwa msimu baada ya kutofautiana na David Moyes kwa kusema
atamalizia maisha yake yaliyobaki katika soka ya ushindani akiwa Old
Trafford.
Van
Persie aliiongoza United kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England katika
msimu wake wa kwanza uliopita baada ya kununuliwa kwa Pauni Milioni 24
kutoka Arsenal, lakini amekuwa akisotea kucheza kwa kiwango chake tangu
Moyes achukue nafasi ya Sir Alex Ferguson.
Imezalisha
maoni kwamba mshambuliaji huyo wa Uholanzi anaweza kuuzwa mwishoni mwa
msimu na Moyes amepanga kukisuka upya kikosi chake kwa kusajili nyota
kadhaa akiweo Edinson Cavani.
![Robin reliant: Van Persie is still Manchester United's main striker despite a difficult season](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/03/13/article-2580100-1C40B74B00000578-215_306x423.jpg)
![Getting stuck in: The Dutchman flies into a tackle in training](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/03/13/article-2580100-1C40BBEE00000578-166_306x423.jpg)
Robin haondoki: Van Persie bado ni mshambuliaji chaguo la kwanza Manchester United licha ya kuwa na msimu mgumu
But
Van Persie mwenye umri wa miaka 30, amesema anataka kuona kumalizia
miaka miwili iliyobaki katika mkataba wake na pengine akafuata nyayo za
Wayne Rooney kwa kusaini Mkataba mpya.
"Ukweli
ni kwamba, nina furaha sana hapa katika klabu,"alisema katika mahojiano
maalum kuelekea mchezo dhidi ya mahasimu Liverpool Jumapili.
"Nimesaini
miaka mnne na nitafurahi kubaki kwa muda mrefu, zaidi ya miaka miwili
niliyobakiza katika Mkataba wangu. Hivi ndivyo ninavyohisi,"amesema.
Imekuwa ikielezwa kwamba Van Persie amesikitishwa na kustaafu kwa Ferguson na havutiwi na mfumo wa mazoezi ya Moyes.
No comments:
Post a Comment