Kuna
msemo unasema, uchungu wa mwana aujuyae mzazi. Hapa pia niseme uchungu
wa kujifungua, aujuaye ni mama. Na furaha ya ufufuo anaijua hasa
aliyefiwa. Tukio mojawapo lililotokea nchini Canada, ambapo mama wa
watoto watatu, alikuwa anatarajia kupata mtoto wake wa nne, binti -
lakini hali ikawa tofauti siku hiyo.
Akiwa ameingizwa ndani kwa ajili ya kujifungua, alikuwa akiamini ya
kwamba mambo yote yatakiwa sawa, hadi pale ambapo alijifungua mtoto,
ambaye hakuwa na uwezo wa kupumua. Mtoto akatamkwa kwamba ni mfu,
daktari akajiridhisha, na manesi wakaondoka nae.
Mama huyo, Robin Cyr mwenye umri wa miaka 34, alikuwa ameongozana na
shangazi yake, ambaye alitambua hali hiyo na kumueleza - kisha akaanza
kuomba.
Majonzi yakiwa yamemtawala Bi. Cyr kwa dakika 28, akiwa kwenye hali ya
maombolezo, ghafla aliona nesi mmoja amerudi ndani huku akiwa kama
amepigwa na bumbuwazi asiweze kuongea neno lolote, akifuatiwa na nesi
mwingine dakika mbili baadae ambaye aliweza kusema kwa ufupi, "mtoto wako ameanza kupumua."
Daktari akaja kuthibitisha, kwa kutanguliza kuomba msamaha kwanza. "Samahani, nilikata tamaa juu ya mtoto wako, na nikampa mgongo kabisa, naye akaanza kupumua mwenyewe - ni muujiza."
Robin Cyr ameelezea kuwa shangazi yake ambaye ni muombaji sana, ndio
amepelekea hali hiyo, na kwamba kwa sasa inabidi atumie muda mrefu
kutafakari jina la kumpa binti yake huyo, kwani dakika 28 za kutokuwa
hai baada ya miezi tisa si suala dogo, ni mkono wa Mungu pekee, na hata
kila mtu anasema kuwa mtoto huyu amefufuka kwa kusudi maalum la Mungu.
No comments:
Post a Comment