BABU mwenye umri wa miaka (80), Benedict mkazi wa Tandika
Kilimahewa, jijini Dar ametiwa mbaroni kwa madai ya kumbaka mjukuu wake
wa kike (jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka (6).
Tukio hilo la kuhuzunisha linadaiwa kutokea Machi 8, mwaka huu usiku
wakati babu na mjukuu wake huyo wakiwa wamelala pamoja chumbani kwake.
Akizungumza na mwandishi wetu, jirani wa babu huyo ambaye hakupenda
jina lake liandikwe gazetini alidai kwamba aliyegundua mtoto huyo
kabakwa ni mjumbe wa nyumba kumi wa eneo analoishi mtuhumiwa
anayefahamika kwa jina la Bibi China.
“Sisi hatukuwa na habari ila mjumbe wetu aliposikia watoto wakisema
nguo ya ndani ya mwenzao (mtoto aliyebakwa) ilikuwa na damu alimwita na
kumkagua, alipomuuliza alipatwa na nini akamwambia babu yake alimfanyia
mchezo mbaya,” alidai jirani huyo.
Mama wa mtoto aliyebakwa.
Aliongeza kuwa, baada ya kumhoji kwa kina, mtoto huyo alisema kuwa
usiku akiwa amelala na babu yake alimvua nguo na kuanza kumfanyia
kitendo hicho.
Jirani huyo alidai kwamba, mtoto aliwaambia kutokana na maumivu
makali aliyopata alipiga mayowe ya kuomba msaada lakini babu yake
aliongeza sauti ya redio hadi mwisho ili watu wasisikie.
Mjumbe wa nyumba kumi wa mtaa huo, Bibi China alikiri kutokea tukio hilo na kuongeza kuwa mtuhumiwa ambaye hana mke alikuwa akilala kitanda kimoja na mjukuu wake huyo.
Mjumbe wa nyumba kumi wa mtaa huo, Bibi China alikiri kutokea tukio hilo na kuongeza kuwa mtuhumiwa ambaye hana mke alikuwa akilala kitanda kimoja na mjukuu wake huyo.
Mtoto aliyefanyiwa unyama huo akizungumza kwa huzuni na paparazi wetu alisema:
“Nilikuwa nimelala nikashtuka navuliwa nguo na babu na kuanza kunibaka, ilikuwa usiku wa manane, nililia lakini yeye aliongeza sauti ya redio ili watu wasisikie nikanyamaza, asubuhi bibi ndiyo akaniona halafu mama akanipeleka hospitali.”

Mama mzazi wa mtoto huyo, Sikwambii Mateo akizungumza na paparazi wetu kuhusiana na tukio hilo alisema:
“Kitendo alichofanyiwa mwanangu na baba yangu mzazi kimeniumiza sana
na imekuwa vigumu kuamini kwa umri aliokuwa nao kama angeweza kufanya
kitendo cha kikatili kwa mjukuu wake na kudai anasingiziwa,
nilipompeleka Hospitali ya Temeke alipochunguzwa alikutwa na manii,”
alisema mama huyo.
Babu huyo mpaka sasa anashikiliwa na Polisi wa Kituo cha Kilimahewa kwa RB namba KLH/RB/236/2014 KUBAKA
Babu huyo mpaka sasa anashikiliwa na Polisi wa Kituo cha Kilimahewa kwa RB namba KLH/RB/236/2014 KUBAKA
No comments:
Post a Comment