KLABU
ya Manchester City imeondoka leo England kwenda Hispania kukamilisha
kile ambacho mbele ya wengi ni mpango usiowezekana, itakapomenyana na
Barcelona Uwanja wa Camp Nou kesho.
Timu
ya Manuel Pellegrini inatakiwa kukipiku kipigo cha mabao 2-0
walichopata Uwanja wa Etihad kutoka kwa Barcelona katika mchezo wa
kwanza wa Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wanakwenda kutolewa? Manuel Pellegrini akiwasili Uwanja wa Ndege wa Manchester tayari kwa safari ya Barcelona
Samir Nasri, Yaya Toure, Vincent Kompany na Sergio Aguero ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa Man City
No comments:
Post a Comment