CHELSEA
imetanua mbawa zake kileleni mwa Ligi Kuu ya England, kufuatia ushindi
wa mabao 4-0 dhidi ya Tottenham Hotspur Uwanja wa Stamford Bridge usku
huu.
Mabao ya The Blues leo yamefungwa na Samuel Eto'o dakika ya 56, Edin Hazard dakika ya 60 na Demba Ba mawili dakika za 88 na 89.
Ushindi
huo, unaifanya Chelsea itimize pointi 69 baada ya kucheza mechi 28 na
kujiimarisha kileleni, ikiizidi kwa pointi saba Liverpool iliyo nafasi
ya pili kwa pointi zake 59 sawa na Asrenal, nao wakiwa wamecheza mechi
28 pia. Manchester City ni ya nne sasa kwa pointi zake 57, lakini ina
mechi mbili mkononi.
Mimi kizee; Eto'o akishangilia kama mzee baada ya kufunga kuwabeza wanaomuita mzee kwenye timu hiyo, baada ya kocha Jose Mourinho pia kusema ana umri mkubwa |

Eto'o akitumia mwili wake kumtoka Michael Dawson

Samuel Eto'o akimzunguka kipa Lloris

Eto'o alianguka mara kadhaa leo
No comments:
Post a Comment