KLABU
ya Inter Milan imetenga dau la Pauni Milioni 20 kumsajili Fernando
Torres ambazo Chelsea wanaweza kuzihitaji ili kumtoa mshambuliaji huyo
anayeshikilia rekodi ya kusajiliwa kwa bei kubwa England.
Torres
amebakiza zaidi ya miaka miwili katika mkataba wake unaomfanya alipwe
mshahara Pauni 150,000 kwa wiki aliosaini miaka mitatu iliyopita kutoka
Liverpool kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 50 na Jose Mourinho
anaweza kusajili mchezaji wa bei mbaya kuziba nafasi yake.
Mmiliki
mpya wa Inter mfanyabiashara wa Indonesia, Erick Thohir amesema
hatapoteza mamilioni mengi katika kuijenga upya timu, lakini amemsaidia
kocha Walter Mazzarri Januari kwa kumpa Pauni Milioni 17 kumsajili
Hernanes.
Wawakilishi
wa klabu hiyo ya Italia walikuwa kwenye mazungumzo na Chelsea wakati wa
usajili wa Januari juu ya Juan Mata na kuwapa ofa ya kuwarejeshea Fredy
Guarin. Hata hawakufanikiwa baada ya Mata kuuzwa Manchester United na
sasa Wataliano hao wamerudi tena kujaribu kumpata Mspanyola mwingine,
Torres.
Suala la Torres linafuatia Inter kutangaza kumsajili Nahodha wa Manchester United, Nemanja Vidic kwa ajili ya msimu ujao.
Klabu
hiyo ilithibitisha kumpata mchezaji huyo Jumatano na picha ya Vidic
ikapostiwa kwenye ukurasa wa Twitter wa Inter sambamba na ujumbe: "Hapa
ni Vidic akisaini Mkataba. Tutakuona Juni, Nemanja!'
Makubaliano
yaliyofikiwa ni ya misimu mitatu ambao utamfanya Vidic astaafu vizuri
kwa maana ya hadhi na maslahi akiwa na klabu nyingine kubwa Ulaya.
No comments:
Post a Comment