Wajumbe wa Bunge la Katiba, wakimwondoa mwenzao baada ya kutokea vurugu
bungeni jana wakati Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
akijiandaa kuwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba. Picha na Emmanuel
Herman
******
Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta jana alipata
jaribio la kwanza baada ya baadhi ya wajumbe kupinga kuruhusiwa kwa
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba
kuwasilisha Rasimu ya Katiba kwa madai ya ukiukwaji wa kanuni za Bunge.
Wajumbe hao chini ya Umoja wa Katiba ya Watanzania
(Ukawa), walitangaza mapema jana kwamba wangepinga ratiba nzima
kuendelea hadi madai yao ya kumtaka Rais Jakaya Kikwete afungue Bunge
kwanza kabla ya rasimu kuwasilishwa yasikilizwe.
No comments:
Post a Comment