MWANASOKA
bora wa dunia, Cristiano Ronaldo jana ameifungia mabao mawili Ureno
ikiitandika 5-1 Cameroon katika mchezo wa kirafiki na kuwa mchezaji
aliyeifungia mabao mengi zaidi Ureno kihistoria.
Ronaldo sasa amefikisha jumla ya 49 aliyoifungia Ureno, mawili zaidi ya Pauleta aliyekuwa anaongoza.
"Sina
wasiwasi wa kuvunja rekodi, ni vitu ambavyo vinakuja vyenyewe, kwa
baraka tele", alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 akihojiwa na
Televisheni ya RTP.
Cameroon
ilimaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza ikiwa imefungana bao 1-1 na
Ureno, lakini kipindi cha pili ikabugizwa nne ndani ya dakika 18.
Ronaldo
alianza kufunga dakika ya 21, Aboubakar akaisawazishia Cameroon dakika
ya 43 na kipindi cha pili Meireles akaifungia Ureno dakika ya 66,
akifuatiwa na Coentrao dakika ya 67, Edinho dakika ya 77 na Cristiano
tena dakika ya 83.
Nani mwingine? Cristiano Ronaldo akishangilia bao lake la kwanza jana dhidi ya Waafrika
No comments:
Post a Comment