Amesajiliwa: James Rodriguez ametambulishwa Real Madrid leo na kukabidhiwa jezi mamba 10 Uwanja wa Santiago Bernabeu
MFUNGAJI
bora wa Kombe la Dunia, James Rodriguez hatimaye ametambulishwa Real
Madrid baada ya kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 60 kutoka Monaco
jioni ya leo.
Mwanasoka
huyo wa kimataifa wa Colombia amesaini mkataba wa miaka sita na Madrid
baada ya kufuzu vipimo vya afya asubuhi Santiago Bernabau na kukabidhiwa
jezi namba 10.
Rais
wa Madrid, Florentino Perez amemkaribisha mshambuliaji huyo
akimfananisha na gwiji wa zamani wa klabu hiyo, marehemu Alfredo Di
Stefano ambaye pia alijiunga na klabu hiyo akitokea Colombia.

Rais wa Real Madrid, Florentino Perez (kushoto), Rodriguez (kulia) na mkewe Daniela wakati wa kutambulishwa

Rodriguez akionyesha uwezo mbele ua maelfu ya mashabiki uwanjani


Rodriguez alionyesha uwezo mkubwa Bernabeu

Rodriguez alikonga nyoyo za mashabiki kwa vita hivi
No comments:
Post a Comment