MAKAMU MWENYEKITI MTENDAJI wa Manchester United, Ed Woodward,
amewaambia Mashabiki wa Klabu hiyo kuwa wategemee ujio wa Wachezaji
wapya kadhaa na pia kuhama kwa baadhi ya Wachezaji katika Wiki chache
zijazo.
United imetumia Pauni Milioni 50 kuwanunua Luke Shaw na Ander
Herrera na kauli hii ya Woodward inaleta imani kuwa Meneja mpya Louis
van Gaal atapata Wachezaji wengine wapya kabla Msimu mpya kuanza.
Kwa sasa, Wachezaji wanaohusishwa kuhamia Man United ni pamoja na
Arturo Vidal, Daley Blind, Kevin Strootman na Thomas Vermaelen.
Woodward ametamka: “Hamna kiwango cha Bajeti kilichowekwa. Kifedha
tuna nguvu sana, zipo Fedha za Uhamisho. Louis ndie Bosi na anatathmini
nini kinaendelea lakini tumekuwa na mazungumzo na walengwa na kazi
inaendelea nyuma ya pazia. Tunasonga mbele kwa baadhi ya walengwa
hao…hivyo kaeni chonjo hapa!”
Aliongeza: “Louis anapata muda zaidi wa kufanya tathmini yake na
ikibidi tutabadilisha maamuzi na kufanya mengine. Tunataka kuchukua
hatua thabiti ili kutwaa Ubingwa!”
Msimu uliopita Man United walimaliza Nafasi ya 7 kwenye Ligi Kuu
England na hivyo Msimu ujao hawatashiriki Mashindano ya Klabu Barani
Ulaya, ikiwa ni mara ya kwanza tangu 1996, lakini Woodward amedai hilo
haliathiri wao kupata Wachezaji wapya.
Ameeleza: “Nimeongea na Mawakala na Wachezaji wengi na sisi bado ni
kivutio kikubwa kwa Wachezaji Dunia nzima. Hilo halina wasiwasi. Tayari
tumeshapata Wachezaji wawili hodari kabisa!”
USA-ZIARA YA KABLA MSIMU MPYA:
[Zote Nchini Marekani]
**Saa za Bongo
Jumatano 24 Julai 2014, Rose Bowl, Pasadena
0606 Manchester United v LA Galaxy
Chevrolet FC Cup
Jumamosi 26 Julai 2014, Sports Authority Field, Denver
2306 Manchester United v AS Roma
International Champions Cup
Jumanne 30 Julai 2014 [Usiku wa 29 kuamkia 30], FedEx Field, Washington DC
0230 Manchester United v Inter Milan
International Champions Cup
Jumanne 02 Agosti 2014, Michigan Stadium, Ann Arbor
2306 Manchester United v Real Madrid
International Champions Cup
Jumanne 12 Agosti 2014, Old Trafford
REUNITED14
2130 Manchester United v Valencia
Jumanne 12 Agosti 2014, Old Trafford
Ligi Kuu England
1445 Man United v Swansea City
No comments:
Post a Comment