Thursday, 10 July 2014

SIMBA SC YAFANYA KUFURU, YASAINI WATATU KWA MPIGO LEO AKIWEMO MANYIKA JR. NA BEKI LA MWADUI

SIMBA SC imesajili wachezaji wawili chupukizi
kwa ajili ya timu yake ya vijana chini ya umri wa
miaka 20, maarufu kama Simba B, akiwemo
Peter Manyika, mtoto wa kipa wa zamani wa
Yanga SC, Manyika Opeter.
Makamu Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange
‘Kaburu’ amesimamia zoezi hilo lililokamilika
vyema akishirikiana na Mjumbe wa Kamati ya
Usajili, Said Tuliy leo mjini Dar es Salaam.
Pamoja na kipa huyo wa timu ya taifa ya vijana
chini ya umri wa miaka 20, Simba SC pia
imemsajili kinda mwingine kutoka Mwadui ya
Shinyanga, Ibrahim Hajibu Migomba.
Kaburu maarufu kama Perez, amesema mtoto
wa Manyika amesaini miaka mitatu sawa na
Hajibu ambao wote pamoja na kusajiliwa kama
wachezaji wa Simba B, watakuwa wanakomazwa
kikosi cha kwanza.
Awali ya hapo, leo Simba SC ilimsajili kipa wa
Mtibwa Sugar ya Morogoro, Hussein Sharrif
‘Cassilas’ aliyesaini Mkataba wa miaka miwili.
Kipa huyo bora wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara amekuwa akiibeba Mtibwa Sugar
kwa misimu mitatu iliyopita, tangu kuondoka
kwa Shaaban Hassan Kado.

No comments:

Post a Comment