Dar na Marekani. Gavana wa zamani wa
Benki Kuu ya Tanzania BOT), Marehemu
Daudi Ballali aliacha wasia unaotaka maiti
yake isionyeshwe hadharani atakapofariki
dunia na wala maiti yake isiletwe Tanzania
kwa ajili ya maziko.
Ballali aliyefariki Mei 16, 2008 na kuzikwa Mei
23 mwaka huohuo katika makaburi ya Gate
of Heaven, eneo la Silver Spring, Maryland
nchini Marekani alifahamu kuhusu kifo chake
wiki mbili kabla, baada ya matibabu
kushindikana.
Mwandishi wa Mwananchi aliyekuwa nchini
Marekani kwa siku kumi kufuatilia suala hilo,
alibaini kuwa kiongozi huyo alilazwa mara ya
pili katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha
George Washington, April 2008 na alirejea
nyumbani kwake, Washington DC wiki mbili
kabla ya kukutwa na mauti.
Habari kutoka ndani ya familia yake
zinasema baada ya madaktari kushindwa
kumtibu walimwambia kwamba asingeweza
kuishi kwa zaidi ya wiki mbili, hivyo
walimshauri ahamie kwenye ‘hospice’
ambayo ni nyumba maalumu ya kusubiri kifo
kwa watu ambao magonjwa yao
yameshindikana.
Hospice hutumika kwa ajili ya kuwaweka
wagonjwa wanaohitaji faraja hasa kutoka na
maumivu makali chini ya uangalizi wa
washauri na wauguzi kwa lengo la
kuwaongezea wagonjwa husika siku za
kuishi.
Baadhi ya hospice hutoa huduma za kiroho,
kijamii na kifedha na wakati mwingine
huduma hizo hutolewa kwa wagonjwa ambao
wanaugulia nyumbani. Hata hivyo, gazeti hili
lilidokezwa kwamba Ballali alikataa kwenda
kwenye nyumba hiyo na badala yake kutaka
apelekwe nyumbani kwake.
“Alikataa kwenda kwenye hospice,
aliwaambia madaktari kwamba yeye hawezi
kwenda huko ijapokuwa kuna huduma nzuri
na uangalizi wa nesi (muuguzi). Aliwaambia
kwamba nitakwenda kufia nyumbani kwangu
maana nina nyumbani kwangu,” kilisema
chanzo chetu na kuongeza:
“Aliporejeshwa nyumbani, alikuwa
anazungumza kama kawaida lakini kadri siku
zilivyosogea hali ilikuwa ikibadilika na kama
sikosei siku mbili au tatu za mwisho (za uhai
wake) alikuwa anajitambua lakini alikata
kauli, hakuwa akizungumza chochote”.
Uchunguzi wetu umebaini kuwa katika siku
hizo za mwisho za uhai wake, Ballali aliacha
maelekezo kwamba pindi atakapofariki dunia,
mwili wake usiwekwe hadharani kwa maana
ya kutazamwa na watu nje ya familia wala
kusafirishwa kuja Tanzania kwa ajili ya
maziko.
“He said, he doesn’t like to be turned into a
laughing staff (alisema asingependa
kugeuzwa kichekesho), sababu watu
wasingekuja kutoa heshima za mwisho, bali
wangekuja kumdhihaki kuangalia Ballali
aliyetuhumiwa kwa ufisadi wa EPA na siyo
Gavana,” kilisema chanzo hicho.
Monday, 14 July 2014
SEHEMU YA PILI .. Kauli ya Mwisho ya Ballali Kabla ya Kifo Chake
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment