MENEJA wa England Roy Hodgson amewaongoza Magwiji wa Soka wengi huko
Uingereza kummiminia sifa aliekuwa Nahodha wa England Steven Gerrard
mara baada ya kutangaza kustaafu kuichezea Nchi yake.
Gerrard, mwenye Miaka 34 na ni Nahodha wa Liverpool, aliichezea England Mechi 114 na kufunga Bao 21 na kuiwakilisha katika Mashindano makubwa 6.
Gerrard, ambae amekuwa Nahodha wa England mara 38, ndie Mchezaji wa 3 kwa kuichezea England mara nyingi akiwa nyuma ya Kipa Peter Shilton, Mechi 125, na David Beckham, Mechi 115.
Roy Hodgson amesema England itaukosa uongozi madhubuti wa Gerrard wakati wana Kikosi kichanga.
Nae Nahodha wa zamani wa England, Bryan Robson, ambae pia alikuwa Nahodha wa Manchester United, amesema Gerrard amekuwa Mtumishi mwema kwa Nchi yake.
Gary Lineker, Straika wa zamani wa England na sasa Mchambuzi wa BBC, ameeleza Gerrard ni Mtumishi mwema na Mchezaji mahiri aliejituma kwa kila kitu kwa Nchi yake.
Mchezaji wa zamani wa Liverpool na England, Jamie Carragher, ambae ni Rafiki wa karibu wa Gerrard, ameeleza: “Ni uamuzi mzuri wa Gerrard, Mechi 114, ni Mtumishi bora kwa England!”
Michael Owen, Fowadi wa zamani wa England, Liverpool na Man United, ameeleza England itamkosa sana Gerrard.
Nahodha wa zamani wa England na Mchezaji wa zamani wa Man United, Rio Ferdinand, aliposti kwenye Twitter na kumueleza Gerrard kama Mchezaji hodari ambae anastahili pongezi kwa kuichezea England zaidi ya Mechi 100.
Gerrard, ambae alianza kuichezea England Mwaka 2000 kwenye Mechi waliyoifunga Ukraine 2-0, aliichezea England kwa mara ya mwisho huko Brazil Mwezi uliopita walipotoka Sare 0-0 na Costa Rica kwenye Mechi ya Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia.
Akitangaza habari hizi za kustaafu kwake kuichezea England, Gerrard alisema: “Nilisikia raha muda wote niliochezea Nchi yangu. Hii ni Siku ya huzuni kwangu.”
Gerrard ataendelea kuichezea Klabu yake Liverpool ambayo alicheza nao Mechi yake ya kwanza kabisa Mwaka 1998 dhidi ya Blackburn Rovers.

No comments:
Post a Comment