Tuesday, 15 July 2014

DIEGO COSTA AMUAHIDI MOURINHO MATAJI BAADA YA KUSAINI MKATABA WA MITANO CHELSEA

MSHAMBULIAJI Diego Costa amepania kushinda mataji zaidi baada ya kukamilisha usajili wake Chelsea.
Mzaliwa huyo wa Brazil, aliiwezesha Atletico Madrid kutwaa taji la La Liga msimu uliopita, na kuifikisha Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya walipofungwa na Real Madrid.
Jose Mourinho alishindwa kutwaa taji lolote katika msimu wake wa kwanza wa kurejea Stamford Bridge, lakini Costa anajiamini anaweza kumsaidia kutimiza ndoto hizo baada ya kutua magharibi mwa London.  
d

"Nina furaha sana kusaini Chelsea. Kila mtu anajua ni klabu kubwa katika livi ya ushindani sana, na ninavutiwa sana kuanza Ligi Kuu England na kocha babu kubwa na wachezaji wenzangu. Nikiwa nimecheza dhidi ya Chelsea msimu uliopita ninafahamu ubora wa kikosi ninachojiunga nacho,"amesema mchezaji huyo wa Hispania, anayetua Chelsea kwa dau la Pauni 32 kwa Mkataba wa miaka mitano.
Taarifa ya Chelsea imesema; "Klabu ya Chelsea inayo furaha kutangaza kwamba Diego Costa leo amekamilisha uhamisho wake kutoka Atletico Madrid kwa kusaini Mkataba wa miaka mitano. Atajiunga na kikosi cha kwanza wiki ijayo kwa ajili ya ziara ya Ulaya kujiandaa na msimu," .

MAN UNITED YANASA MAKINDA WAWILI WENYE MIAKA 15 KUTOKA BENFICA, JOAO FILIPE NA JOAO VIRGINIA KWA LENGO LA KUWAFANYIA MAJARIBIO Kimataifa

article-0-1FA9449000000578-532_634x417
Kinda mkali: Joao Filipe (wa pili kulia) akiwa katika gari kuelekea uwanja wa mazoezi wa Manchester United wa Carrington.
MANCHESTER United imewachukua wachezaji wawili wenye umri wa miaka  15 kutoka Benfica kwa lengo la kuwafanyia majaribio.
Winga mwenye thamani kubwa,  Joao Filipe aliwasili  katika uwanja wa mazoezi wa United wa Carrington jana jumanne  na kutazamwa na makocha wa timu hiyo.
Mchezaji mwingine aliyechukuliwa kwa majaribio ni mlinda mlango, Joao Virginia.
 
Mashetani wekundu watamfanyia majaribio Filipe kwa miezi sita na tayari kinda huyo alisharipotiwa kuwindwa na Barcelona.
 JOAO FILIPE NI NANI?
Umri: 15
Kimo: 5ft5in
Nafasi: Winga, anaweza kucheza sehemu yoyote ya ushambuliaji
Klabu ya sasa: Benfica
Anaowapenda: Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Neymar
TIMU NYINGINE ZINAZOMTAKA Barcelona, Real Madrid, Chelsea, Liverpool, Arsenal 
Benfica inahangaika kuwasainisha mikataba ya muda mrefu nyota hao wawili, lakini inakabiliana na changamoto kubwa kutoka duniani kote.
Wachezaji wengi makinda wamekuwa wakichukuliwa na United, lakini hawadumu.
Japokuwa kwa hawa wawili, United wana msimamo wa kuwasajili mapema kutokana na Filipe na Viriginia kuwa miongoni mwa wachezaji wakali vijana nchini Ureno siku za karibuni.
Walipoulizwa kuhusu wachezaji hao wawili, United walisema kamwe hawazungumzi lolote juu ya wachezaji wanaofanya majaribio klabuni hapo. 
Hidden from view: 'The next Cristiano Ronaldo' (centre) made a low-key entrance in a Range Rover
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=3546#sthash.goPPgHwz.dpuf

No comments:

Post a Comment