Wednesday, 30 July 2014

RASMI, EVERTON WAJIBEBEA JUMLA LUKAKU KWA PAUNI MILIONI 28

Dili limetiki: Mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji, Romelu Lukaku akiwa ameshika jezi ya Everton pamoja na kocha Roberto Martinez jana, baada ya kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 28 kutoka Chelsea. Lukaku alijiunga na Chelsea misimu mitatu iliyopita lakini akaambulia kucheza mechi 10 tu za Ligi Kuu England Stamford Bridge kabla ya kutolewa kwa mkopo West Brom na baadaye Everton anakohamia jumla.

No comments:

Post a Comment