Beki was Aston Villa Ron Vlaar, 29, atakuwa na
mazungumzo na meneja wake Paul Lambert
kuhusiana na hatma yake licha ya Southampton
kumwania (Daily Mirror), QPR wanafikiria
kumchukua kiungo wa Colombia Carlos
Sanchez, 28, kwa pauni milioni 4 kutoka Elche
(Daily Mirror), West Ham na QPR wamepanda
dau kwa Marseille kumchukua Matheiu
Valbuena baada ya kiungo huyo Mfaransa
kukataa kuhamia Dynamo Moscow (L'Equipe),
Manchester United na Barcelona bado
wanamfuatilia Juan Cuadrado, 26, wa Fiorentina
lakini huenda wakatishwa na bei ya pauni
milioni, 32, ya kiungo huyo kutoka Colombia
(Marca), Manchester United wamefikia
makubaliano "ya mdomo" na kiungo wa
Juventus Arturo Vidal, 27, ya uhamisho wa
pauni milioni 47 (Tuttosport), matumaini ya
Manchester City kumsajili beki kutoka Morocco
Mehdi Benatia, 27, yamefifia baada ya Roma
kusema hakuna dalili za mchezaji huyo
kuondoka (Le Figaro), meneja mpya wa
Manchester United amewaonya mashabiki wake
kuwa timu hiyo huenda ikasuasua katika miezi
mitatu ya mwanzo wa msimu wakati wachezaji
wakianza kuzoea mbinu zake (Times), Van Gaal
amesema iwapo watashinda Ligi Kuu msimu
ujao na kuwapiku majirani zao Manchester City,
utakuwa ushindi "mtamu" zaidi (Manchester
Evening News), kiungo wa Manchester City
Yaya Toure, 31, amesema huenda akasalia
katika timu hiyo hadi atakapoacha kucheza
soka (Guardian), mshambuliaji mpya wa
Barcelona Luis Suarez, 27, ambaye anatumikia
adhabu ya miezi minne, amehamia katika mji
wa Pyrenees kuanza mazoezi ya msimu mpya
akiwa na mwalimu binafsi (Daily Mail), Didier
Drogba, 36, amesema Diego Costa, 25, atakuwa
mchezaji "mkali" katika Ligi Kuu ya England
(Sun), AC Milan wanafanya mazungumzo wa
mshambuliaji kutoka Brazil Robinho, 30 (Le
Figaro), kiungo wa Arsenal Santi Cazorla,29,
bado anasakwa na Atlètico Madrid. Atlètico pia
wanamfuatilia Fernando Torres, 30, na winga
wa PSV Eindhoven Zakaria Bakkali, 18
(AS.com), kiungo anayefuatiliwa na Liverpool,
Xeridan Shaqiri, 22, huenda akaamua kubakia
na klabu yake ya Bayern Munich (Tuttosport),
Borussia Dortmund na Schalke wanamtaka
mshambuliaji kutoka Serbia, Aden Ljajic, 22,
kutoka AS Roma (Bild), Barcelona wametangaza
kumsajili kiungo kutoka Brazil, Alex Varoneze
Dione anayejulikana kama "Betri" kwa miaka
mitatu (Mundodeportivo), Manchester United
wameanza tena kumfuatilia beki wa kati wa
Atletico Madrid Miranda, baada ya Atlètico
kusema wapo tayari kupokea dau la pauni
milioni 23 (Metro), AC Milan wanamtaka winga
wa Newcastle Hatem Ben Arfa na huenda
akauzwa kwa pauni milioni 12 (Daily Star),
Bayern Munich wapo tayari kusubiri hadi Oktoba
kumsajili kipa wa zamani wa Barcelona Victor
Valdez ambaye anauguza jeraha la goti, ingawa
anaweza kusita kwenda kugombea namba na
Manuel Neuer (Mundo Deportivo), QPR
wanataka kumchukua Ronaldinho ambaye
amemaliza mkataba wake na Atletico Mineiro
(Globoesporte) na Chelsea wanakataa
kutengeneza jezi zenye jina la kipa Thibaut
Courtois, 22 na Romelu Lukaku, 22, kwa sababu
wachezaji hao bado hawajapewa namba (Daily
Star). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Share
hizi na wapenda soka wote. Cheers!!!
Wednesday, 30 July 2014
TETESI ZA SOKA ULAYA..MAN U WAMEFIKIA MAKUBALIANO KUMSAJIRI VIDAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment