BIA
ya Castle Lager, bia inayoongoza barani Afrika na FC Barcelona, moja
kati ya timu kubwa zaidi za soka duniani wameshirikiana kuleta makocha
kutoka klabu hiyo yenye makao yake huko Camp Nou, Hispania ili kutoa
mafunzo ya mbinu za soka kwa makocha wa Tanzania wiki hii. Makocha hao
wa FC Barcelona ambao wataendesha mafunzo hayo wamefika jijini Dar es
salaam leo (31/8/2014). Mafunzo
hayo yatafanyika kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam kwa siku
mbili zijazo ambazo ni tarehe 1 na tarehe 2 Agosti na yataendeshwa na
makocha waliobobea kwenye mbinu mbalimbali za kandanda ikiwemo Tiki
Taka.
Makocha hawa ni Daniel Bigas Alsina and Isaac Oriol Guerrero Hernandez kutoka Shule ya Soka ya FB Barcelona.
Mafunzo
haya ni sehemu ya manufaa ya ushirikiano uliosainiwa mwaka jana kati ya
FC Barcelona na Castle Lager ambayo ni bia rasmi ya FC Barcelona barani
Afrika. Vilevile, mafunzo haya ni sehemu ya manufaa ya ushirikiano huu
kwa jamii.
Kupitia
mafunzo haya, makocha 30 waliobahatika kutoka ligi kuu na ligi daraja
la kwanza watapata fursa maalum ya kujifunza mbinu mbalimbali za mazoezi
zinazotumiwa na FC Barcelona na kufanikiwa kuwatengeneza baadhi ya
wachezaji wenye mafanikio makubwa zaidi duniani.
“Tuna
shauku kubwa sana kuona mafunzo haya yanakuja Tanzania na tunafurahia
kupata nafasi ya kurudisha fadhila kwa jamii ambayo inatuunga mkono.
Tunaamini mafunzo haya yatawanufaisha makocha na wachezaji wa Tanzania
katika siku zijazo,” alisema Fimbo Buttallah, Meneja Masoko wa Kampuni
ya Bia Tanzania.
“Castle
Lager ina historia kubwa na soka barani Afrika na tukio hili litazidi
kuimarisha uhusiano uliopo kati ya bia namba moja Afrika na mchezo namba
moja kwa kupendwa barani Afrika.”
Mafunzo
haya kwa makocha yatahusisha mafunzo ya darasani kwa nadharia na
uwanjani kwa vitendo. Ikiwa ni sehemu ya mafunzo hayo, makocha hao
watatoa baadhi ya siri za mafanikio ya FC Barcelona ili kusaidia kuleta
utaalamu wa kimataifa kwenye soka la Tanzania.
No comments:
Post a Comment