Mabingwa wa Spain, Atletico Madrid wanataka
kuwasajili Santi Cazorla, 29, kutoka Arsenal,
Fernando Torres, 30, kutoka Chelsea na
Chicharito, 26 kutoka Manchester United (Daily
Star), Chicharito amekiri kuwa hana uhakika
kama ataendelea kuwepo Old Trafford akisema
"Mungu pekee ndio anajua" kuhusu hatma yake
(Guardian), Tottenham wanatarajia kurejea na
fedha zaidi kumtaka kiungo wa Southampton
Morgan Schneiderlin, licha ya Saints kusema
mchezaji huyo hatoruhusiwa kuondoka (Daily
Telegraph), Sporting Lisbon wamewaambia
Southampton kuwa watalazimika kutoa pauni
milioni 16 kumsajili beki kutoka Argentina Eric
Dier, 20 (Daily Telepgraph), Marouanne Fellaini,
26 amekubali kujiunga na Napoli ya Italia, lakini
Manchester United wanataka pauni milioni 18
kwa mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa pauni
milioni 27.5 mwaka jana (Daily Star), meneja
wa Sunderland Gus Poyet amethibitisha kuwa
wameanza tena mazungumzo ya kumsajili
Fabio Borini, 23, kutoka Liverpool (Daily
Express), Arsenal wanaweza kufufua
mazungumzo ya kumsajili Sami Khedira, 27,
kwa kuwa Real Madrid wanataka kumuuza
kiungo huyo (Daily Mirror), Juventus
wamekubali dau la pauni milioni 47 kutoka
Manchester United kumsajili Arturo Vidal, 27, na
mchezaji huyo wa Chile amekubali maslahi
binafsi na Old Trafford (CaughtOffside),
matumaini ya Newcastle ya kumsajili
mshambuliaji Alexandre Lacazette, 23, kwa
pauni milioni 10 yamegonga mwamba baada ya
mchezaji huyo wa Ufaransa kusaini mkataba
mpya na klabu yake (Newcastle Cronicle),
Napoli wamewapa Manchester United Dries
Mertens kubadilishana na Marouanne Fellaini
(Daily Express), Karim Benzema amekubali
kusaini mkataba mpya na Real Madrid hadi
mwaka 2018 wenye thamani ya euro milioni 7
kwa mwaka (El Confidencial), Bayern Munich
wameanza kumfuatilia winga wa Real Madrid
Angel Di Maria ambaye anasakwa pia na
Manchester United na Paris Saint-Germain
(AS). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Share
na wapenda soka wote.
Thursday, 31 July 2014
TETESI ZA SOKA ULAYA...PAUNI MILLION 47 ZAMPELEKA VIDAL MANCHESTER UNITED
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment