WASANII wa Tanzania wenye mashabiki wengi
Afrika Mashariki, Lady Jay Dee na Diamond
Platinumz, wameitoa Tanzania Kimasomaso kwa
kushinda tuzo moja moja katika tuzo za AFRIMA
(African Muzik Magazine Awards 2014),
zilizofanyika jana Dallas, Marekani.
Kwa mujibu wa mtandao wa African Music
Magazine, Lady Jay Dee alishinda tuzo ya
mwimbaji bora wa kike wa Afrika Mashariki na
Diamond Platinumz alishinda tuzo ya Msanii bora
wa kiume wa Afrika Mashariki.
Hata hivyo, kwa habari ambazo zimeenea
Tanzania na kutajwa kuwa zilizotolewa na meneja
wa Diamond zinaeleza kuwa Diamond ameshinda
tuzo mbili ambayo nyingine ni wimbo bora wa
kushirikiana.
Hali hiyo ilisababisha utata, kwa mashabiki wa
mwanamuziki huyo Diamond Platnamu hali
iliyopelekea mashabiki hao kuhisi kuwa msanii
huyo amewadanganya mashabiki wake.
Lakini kwenye orodha halisi ya mtandao a
AFRIMMA, tuzo ya wimbo bora wa kushirikiana
imeenda kwa Mafikizolo feat Uhuru (Khona).
Kwa mujibu wa maelezo aliyoandika Diamond
kwenye Instagram, inaonesha kama ameshinda
tuzo zaidi ya moja.
“First of all napenda nimshkuru sana Mwenyez
mungu, Mama, Family, My management, kipenzi
changu, Media, bila kuwasahau nyinyi mashabiki
zangu pendwa kwani sikuzote mmekuwa
mkinisupport bega kwa bega kwenye shida na
raha...Niwashkuru pia Wasanii wenzangu toka nje
na ndani ya Tanzania kwani naamini changamoto
tunazopeana ndio zimefanya hadi sasa mziki wetu
ufikie hapa...hakika tunzo hizi si zangu bali ni za
Muziki wa Bongo flavour... Mwisho kabisa
nimshkuru Mh Rais Jakaya Mrisho kikwete kwa
mchango wake wa kila siku katika sanaa yetu!...
Mr President your Son Did it!!!!! #MdogMdogo.”
Monday, 28 July 2014
DUH, KUMBE DIAMOND KAWADANGANYA WATANZANIA KUHUSU KUSHINDA TUZO!!! SOMA HAPA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment