KLABU ya Yanga imembwaga
mshambuliaji wake Mganda,
Khamis Kiiza ‘Diego wa
Kampala’ baada ya kusajiliwa
kwa Wabrazil wawili, Andrey
Coutinho na Geilson Santos
Santana `Jaja`.
Baada ya Jaja kusaini
mkataba wa miaka miwili jana
makao makuu ya klabu ya
Yanga, kulikuwa na utata ni
mchezaji gani atapigwa chini
kati ya Kiiza na Emmanuel
Anord Okwi.
Awali ujio wa Jaja ulielezwa
kuwaweka kitimoto Kiiza na
Okwi, huku mmojawapo
akitakiwa kutolewa kafara.
Taarifa za uhakika ambazo
mtandao huu umezipata ni
kwamba kocha Maximo
amependekeza kuachwa kwa
Kiiza kutokana na ripoti
iliyoachwa na Hans Van Der
Pluijm.
Mzigo huo uliofuatwa chini ya
kapeti unasema kuwa Pluijm
katika ripoti yake
aliyowasilisha kwa viongozi
baada ya kumalizika kwa
msimu uliopita, alisema ili
Emmanuel Okwi acheze Yanga
sc, lazima Kiiza aondolewe.
Kwa kuzingatia mapendekezo
hayo, Maximo amefuata
ushauri huo na sasa Kiiza
rasmi anaondoka Jangwani.
Katika hatua nyingine,
imeelezwa na chanzo cha
uhakika kuwa Maximo
amewabana viongozi wa Yanga
akiwataka wajenge uwanja wa
mazoezi wa Kaunda ili
kuepukana na adhaa
anayoipata.
Maximo amewakazia na
amesema hakuna jinsi, lazima
uwanja huo ujengwe muda huu.
Pia amewataka viongozi
kuboresha vyumba vya jengo
la Jangwani ili wachezaji wote
waishe pale.
Taarifa zinasema, Maximo
amesema haiwezekani timu
kukaa saa mbili kwenye foleni
inapoelekea uwanjani na
kurudi kambini.
Kwa mazingira hayo anataka
wachezaji wake wakae makao
makuu ya Yanga, mitaa ya
Twiga na Jangwani, halafu
uwanja wa Kaunda ujengwe.
Mbrazil, Marcio Maximo
anafahamika kwa kuwa na
msimamo mkali katika mambo
yake.
Tuesday, 22 July 2014
KHAMIS KIIZA ‘DIEGO’ APIGWA CHINI YANGA SC, OKWI KUENDELEA KUWIKA!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment