Tuesday, 8 July 2014

Watu wanane wamejeruhiwa mmoja akiwa hali mahututi kufuatia mlipuko katika mgahawa mjini Arusha

Watu wanane wamejeruhiwa mmoja akiwa hali
mahututi kufuatia mlipuko katika mkahawa mjini
Arusha Tanzania
Mlipuko huo ulitokea Jumatatu jioni na polisi
wangali wanachunguza kilichousababisha.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, mlipuko
huo ulitokea Jumatatu jioni na kuwajeruhi watu
wanane huku mmoja akiwa hali mahututi.
Haijulikani kilichosababisha mlipuko huo.
Kufika sasa afisaa mkuu wa shirika la ujasusi
nchini humo anakutana na wandishi wa habari.
Taarifa zaidi punde tutakapozipata.

No comments:

Post a Comment