Friday, 11 July 2014

JOSE MOURINHO KUMRUDISHA DARAJANI GWIJI WA CHELSEA DIDIER DROGBA

KLABU ya Chelsea inaangalia
uwezekano wa kumrudisha
Didier Drogba katika dimba la
Stamford Bridge.
Nyota huyo mwenye miaka 36
anazivutia klabu za Qatar,
wakati Juventus nao
wakifikiria kumnasa mkongwe
huyo anayecheza katika klabu
ya Galatasaray ya Uturuki.
Bado Jose Mourinho ana
mahusiano mazuri na Muivory
coast huyo na anavutiwa
kumrudisha kwa majukumu ya
ukocha zaidi.
Mkongwe huyu wa miaka 36
anazivutia klabu za Qatar, nao
Juventus wanaitaka saini
yake.
Klabu hizo za Qatar zinatarajia
kutoa ofa nono na mshahara
utajadiliwa, lakini unakadiriwa
kuwa paundi milioni 3 kwa
msimu baada ya makato ya
kodi.
Wazo la kurudi Chelsea
litaangaliwa zaidi na pande
zote.
Mourinho amekuwa na
mapenzi makubwa kwa Drogba
na anajua kuwa atakuwa na
msaada mkubwa katika kikosi
chake msimu ujao.
Alionesha nia hiyo hata
Galatasaray ilipokutana na
Chelsea katika michuano ya
UEFA mwezi machi mwaka huu
na alieleza kuwa Drogba
anaweza kurudi na yuko
makini kufanikisha hilo.
Drogba alishinda makombe
matatu ya ligi, makombe
manne ya FA na kombe la
UEFA akiwa katika klabu ya
Chelsea na Mourinho anataka
kutumia uzoefu wake
kuwashauri wachezaji wake
wapya.

No comments:

Post a Comment