LIVERPOOL
imaifunga kwa penalti 3-1 Manchester City kufuatia sare ya 2-2 ndani ya
dakika 90 katika mchezo wa Kombe la Kimataifa kujiandaa na msimu mpya
Uwanja wa Yankee, Marekani.
Man
City ilipata mabao yake kupitia kwa Stevan Jovetic dakika za 53 na 67
wakati mabao ya Liverpool yalifungwa na kwa Jordan Henderson dakika ya
59 na Raheem Sterling dakika ya 85.
Mikwaju
ya penalti ya Yaya Toure na Jesus Navas iliokolewa na Mignolet wakati
pia Aleksandar Kolarov naye alikosa kwa kupaisha- hivyo kumpa nafasi
Lucas Leiva kuipa ushindi wa 3-1 timu ya Brendan Rodgers. Iheanacho
pekee aliifungia City.
Sturridge pia alipaisha penalti yake, lakini Emre Can na Henderson walifunga kabla ya Lucas kutumbukiza kambani ya ushindi.
Timu
hiyo ya Merseysiders sasa itamenyana na AC Milan mjini Charlotte
Jumamosi ikiwa na nafasi ya kuongoza kundi lake- ili ikutane na
mahasimu, Manchester United inayofundishwa na Louis van Gaal mjini
Miami.
No comments:
Post a Comment