Thursday, 17 July 2014

UMAFIA HADI ULAYA, CHELSEA YAIPINDUA ARSENAL DILI LA KHEDIRA

KLABU ya Chelsea ipo kwenye nafasi nzuri ya
kumsaini Sami Khedira baada ya jana usiku
wakala wake kusema hakuna makubaliano
yaliyofikiwa na Arsenal.
Kocha wa Blues, Jose Mourinho amemsajili beki
wa kushoto Filipe Luis kutoka Atletico Madrid
kwa Pauni Milioni 18 na kuhamishia nguvu zake
kwa kiungo wa Ujerumani, Khedira.
Ilikuwa inafahamika Arsenal ilikubali kutoa Pauni
Milioni 20 kwa Real Madrid kumnunua mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 27, lakini walikuwa
wanasuasua kufika kiwango cha mshahara
anaotaka, Pauni 180,000 kwa wiki.                                                        
Pamoja na hayo, wakala wa Khedira, Jorg
Neubauer amesema: "Hatupo katika
mazungumzo na Arsenal. Sifikiri wanweza
kukubaliana ada, vinginevyo ningeambiwa,".
Khedira anavutiwa na Mourinho tangu
anafundisha Real na kocha huyo inafahamika pia
anampenda sana mchezaji huyo.

No comments:

Post a Comment