Meneja mpya wa Manchester United Louis van
Gaal ameambiwa kuwa anaweza kutumia kiasi
chochote cha fedha kusajili wachezaji wapya
Old Trafford na hata kuvunja rekodi za
uhamisho (Guardian), Man U Pia wametajiwa
kuwa wanaweza kuendelea kumsaka Angel Di
Maria, 26, kufuatia Real Madrid kumsajili kiungo
mshambuliaji James Rodriguez, 23, kutoka
Monaco (Independent), Arsenal wamekubali ada
ya uhamisho ya pauni milioni 3 kumsajili kipa
wa David Ospina, 25 kutoka Nice ya Ufaransa
(Guardian), boss wa Liverpool Brendan Rodgers
anataka kumsajili beki wa kulia Javier
Manquillo, 20, kutoka Atletico Madrid kwa
mkopo. Mchezaji huyo anawindwa pia na
Arsenal (Sun), Atletico Madrid wanawanyatia
wachezaji wawili wa Arsenal, Santi Cazorla na
Nancho Monreal (Daily Telegraph), Arsenal
wamerejea kumyatia kiungo wa Sporting Lisbon
William Carvalho, 22, baada ya mazungumzo ya
kumchukua Sami Khedira wa Real Madrid, 27,
kusuasua (Daily Star), Tottenham na Arsenal
wanaonesha nia ya kumsajili kiungo mshabuliaji
Douglas Costa, 23, kutoka Shakhtar Donetsk.
Mchezaji huyo kutoka Brazil amekataa kurejea
Ukraine kutokana na matatizo ya kisiasa katika
nchi hiyo (Independent), mshambuliaji Divock
Origi, 19, amesafiri kwenda Marekani
kukamilisha usajili wake wa Liverpool, lakini
atabakia Lille kwa msimu ujao (Daily Express),
uwezekano wa Didier Drogba, 36, kurejea
Chelsea huenda kukasababisha Romelu Lukaku
kuondoka Darajani, na huenda akaenda Everton
(Daily Telegraph), Everton wameripotiwa
kukaribia kumsajili David Henen, 18, kutoka
Anderlecht (Liverpool Echo), Inter Milan wako
makini kumsajili mshambuliaji wa Manchester
United Javier Hernandez, baada ya kuambiwa
na Manchester City kuwa Stevan Jovetic, 24,
hauzwi (Sun), Hull City wanazungumza na beki
wa kimataifa kutoka Cameroon Jean-Armel
Kana-Biyik, 25 kutaka kumsajili kutoka Rennes
ya Ufaransa (Sky Sports), Lionel Messi, 27,
'alitishia' kujiunga na Arsenal msimu uliopita,
wakati akizungumzia mkataba wake mpya na
Barcelona (Daily Mail), Luis Suarez, 27,
ameukimbia mji wa Barcelona, kuwaepuka
waandishi wa habari wanaomfuatilia kwa karibu
(Daily Star), Manchester United wanajiandaa
kutoa pauni milioni 39 kumchukua Arturo Vidal,
27, kutoka Juventus (Tuttosport), klabu ya
Eintracht Frankfurt ya Ujerumani imefuta
mazungumzo na mshambuliaji wa zamani wa
Arsenal Nicklas Bendtner, 26, kwa sababu
mchezaji huyo anataka mshahara mkubwa (Le
Figaro), meneja wa Borussia Dortmund Jurgen
Klopp ametupilia mbali tetesi kuwa beki Mats
Hummels, 25, anakwenda Manchester United,
na kiungo Marco Reus, 25 anakwenda Bayern
Munich (Bild), Atletico Madrid wanashindwa
kutoa pauni milioni 13 wanazotaka Chelsea
kumsajili Fernando Torres, 30, licha ya kuwa
meneja Diego Simione kutaka sana kumchukua
(AS). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Share
hizi na wapenda soka wote. Cheers!
Wednesday, 23 July 2014
TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA ZOTE ZIKO HAPA...CHUKUA MDA WAKL KUJUA TIMU YAKO INASAJIRI MCHEZAJI GANI ..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment