![]() |
Wanakuja bongo; Roberto Carlos, Ronaldo Lima, Luis Figo na Zinadine Zidane wanatarajiwa kuzuru na kikosi cha magwiji wa Real Madrid nchini mwezi ujao |
Tuesday, 22 July 2014
KUMEKUCHA ZIARA YA REAL MADRID NCHINI TANZANIA..KIINGILIO CHA CHINI NI SH 5000
KUMEKUCHA.
Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kuhusu ziara ya kikosi cha wachezaji
nyota waliowahi kutamba Real Madrid ya Hispania, maarufu kama Real
Madird Legends ambao watazuru nchini mwezi ujao.
Wachezaji
waliotamba kuanzia La Liga, wakacheza ligi nyingine za Ulaya, Kombe la
Ulaya, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Dunia waliowahi kuchezea Madrid
watakuja nchini Agosti 22.
Katika
ziara hiyo, pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki na kikosi maalum cha
wachezaji nyota wa Tanzania, pia watafanya utalii katika vivutio
mbalimbali, ikiwemo kupanda mlima Kilimanjaro.
Real
Madrid inakuja nchini kwa mwaliko wa kampuni ya Tanzania Sisi ni
Nyumbani (TSN), chini ya Mkurugenzi wake Mkuu, Farough Baghozah na
Meneja ziara hiyo, Dennis Ssebo amesema; “kila kitu safi”.
Ssebo
ameiambia KITOMIXNEWS jana mjini Dar es Salaam kwamba, leo watakuwa na
Mkutano na Waandishi wa Habari, Saa 4:00 asubuhi katika hoteli ya New
Africa, Dar es Salaam kutaja wadhamini wa ziara hiyo.
“Tutazungumza
na Waandishi wa Habari kesho, kutaja makampuni ambayo hadi sasa
yamejitokeza kudhamini ziara hii,”amesema Ssebo ambaye pia ameongeza;
“Kwa ujumla maandalizi yote yanaendelea vizuri,”.
Miongoni
mwa nyota wanaotarajiwa kuja na Real nchini ni pamoja na Wanasoka Bora
wa zamani wa Dunia, Mfaransa Zinadine Zidane, Mreno Luis Figo na
Mbrazil, Ronaldo Lima.
Magwiji hao wa Real tayari wamekwishafanya matangazo ya ziara yao nchini wakisema wana hamu mno ya kukanyaga ardhi ya Tanzania.
Labels:
sports
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment