ALIYEKUWA kocha wa Manchester United, David Moyes anachunguzwa na Polisi kwa tuhuma za kijana wa kiume baa.
Tukio hilo baina ya Moyes, mwenye umri wa miaka 51 na kijana wa miaka 23 inaelezwa lilitokea Clitheroe, Lancashire, majira ya Saa 4:00 usiku Jumatano.
Msemaji wa Lancashire Constabulary amesema leo: "Polisi wanachunguza taarifa ya udhalilishwaji wa kijana katika baa ya Emporium mjini Clitheroe.
"Maofisa walifika katika baa majira ya Saa 4:00 usiku jana na iliripotiwa kwamba kijana wa umri wa miaka 23 alidhalilishwa na mtu mwenye miaka 51. Hakutoa taarifa za hospitali.
Maeneo: Baa ya Emporium iliyopo Clitheroe, Lancashire, ambako Moyes anadaiwa kudhalilisha mtu
Taarifa ya Clitheroe imesema kwamba Moyes alikuwa anapata kilaji na rafiki yake wakati wa tukio hilo baa.
Moyes ni miongoni mea walimu kadhaa wanaohusishwa na kupewa ukocha wa Celtic baada ya Neil Lennon kuachia ngazi jana kwa mabingwa hao wa Scotland.
Mwezi uliopita alifukuzwa Manchester United baada ya matokeo mabaya katika Ligi Kuu ya England.
No comments:
Post a Comment