LICHA ya Taifa stars kuilaza bao 1-0 Zimbabwe katika mechi ya
kwanza ya hatua ya awali kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi
ya kucheza AFCON mwakani nchini Morocco, majirani zao, Uganda The
Cranes wao wameangukia pua.
Uganda walikuwa ugenini nchini Madagascar na wametandikwa mabao 2-1 na kujiweka mazingira magumu ya kusonga mbele.
Katika mchezo huo washambuliaji wawili wa Yanga, Hamis Kiiza na
Emmanuel Okwi walicheza, lakini hawakuwa na ubavu wa kuiepusha Uganda
kula kipigo.
Wachezaji hao walibanwa kwa dakika zote 90 na sasa wanasubiri kufuta matokeo hayo mjini Kampala wiki mbili zijazo.
Katika mchezo mwingine, Kenya wakiwa nyumbani kwao wamefanikiwa
kuilaza bao 1-0 Comoros, hivyo kuhitaji sare au suluhu ugenini ili
kufuzu hatua ya makundi
Katika mchezo mwingine, Msumbiji wakiwa nyumbani, wameiangushia
mvua ya mafuriko Sudan ya kusini baada ya kuitungua mabao 5-0 nna kuweka
mguu ndani -nje kufuzu hatua ya makundi.
Sudan kusini watahitaji kushinda mabao 6-0 katika mchezo wa
marudiano ili kufuzu hatua ya makundi, lakini kwa kiwango walichoonesha
leo, hizo zinaweza kuwa ndoto za mchana, japokuwa mpira unadunda.
Swiziland wamelazimisha sare nyumbani ya bao 1-1 dhidi ya Sierra
Leone, wakati Burundi wakiwa nyumbani wametoka suluhu ya bila kufungana
dhidi ya Botswana.
Jamhuri ya Kati imelamizisha suluhu nyumbani na Guinea Bissau,
huku Libya ikishindwa kutamba nyumbani baada ya kutoa suluhu dhidi ya
Rwanda.
Mechi inayoendelea sasa ni kati ya Liberia na Lesotho na muda huu ni mapumziko ambapo matokoe ni suluhu ya bila kufungana.
No comments:
Post a Comment