Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
TAARIFA kutoka mjini Khartoum nchini Sudani usiku huu ni kwamba
wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya CECAFA
Nile Basin Cup, Mbeya
City fc chini ya kocha mkuu Juma Mwambusi wamefungwa mabao 2-1 na AFC
Leopard ya Kenya katika mchezo uliopigwa kuanzia majira ya saa 2:00
kamili usiku mjini Khartoum.
Bao la Mbeya City fc limefungwa na kiungo mshambuliaji, Deus Kaseke.
Hata hivyo inaelezwa kuwa mchezo huo ulikuwa mzuri kwa timu zote, lakini AFC walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza.
Ushindi huo unawafanya AFC Leopard wakae kileleni mwa kundi B baada ya kufikisha pointi 6.
Endelea kufuatilia mtandao huu, utakupatia habari kamali hivi punde.
No comments:
Post a Comment