Monday, 12 May 2014

REAL YAJITOA RASMI MBIO ZA UBINGWA LA LIGA BAADA YA KUCHAPWA 2-0

MAKOSA mawili ya kizembe ya Sergio Ramos na Xabi Alonso yamevunja matumaini ya Real Madrid kutwaa mataji matatu msimu huu baada ya kufungwa 2-0 na Celta Vigo usiku huu.
Ili kuweka hai matumaini ya ubingwa wa Hispania, maarufu kama La Liga, Madrid walihitaji Barcelona na Atletico Madrid zipunguzwe kasi, lakini wao wameshindwa kutumia vyema furs yao.
Mabao mawili ya Charles dakika ya 33 na 44 Uwanja wa Balaidos, yameipa ushindi Celta Vigo na sasa Real kutwaa La Liga ni ndoto, kwani sasa wanabaki na pointi 84 za mechi 37, nyuma ya Barcelona yenye pointi 86 na Atletico Madrid 89, wote mechi 37 pia.
Hoi; Wachezaji wa Real Madrid wakiwa wameishiwa nguvu baada ya kufungwa bao la pili
Party pooper: Celta Vigo striker Charles scored twice in their 2-0 win against Real Madrid on Sunday
Mbaya wao: Mshambuliaji wa Celta Vigo, Charles ndiye amefunga mabao yote

No comments:

Post a Comment