Leo hii Diamond Platnumz ameingia kwenye stori nyingine kubwa ya dunia baada ya kuchaguliwa kushiriki kwenye tuzo za Television kubwa ya Marekani ya BET ambapo yupo kwenye kipengele cha wanaogombea BEST INTERNATIONAL ACT AFRICA.
Anaigombea hiyo tuzo na Davido wa Nigeria, Mafikizolo wa South Africa, Tiwa Savage wa Nigeria, Toofan na Sarkodie wa Ghana. the OFFICIAL
BET kupitia page yao ya twitter waliandika kuthibitisha kuchaguliwa kwa Diamond na kumpongeza akiwa pia ni msanii pekee wa Afrika Mashariki kwenye tuzo hizi za mwaka huu.
![BET DIAMOND PLATNUMZ 2014](http://i2.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/05/BET-DIAMOND-PLATNUMZ-2014.png?resize=507%2C314)
No comments:
Post a Comment