GIGGS AKUTANA NA VAN GAAL KUJADILI HATIMA YAKE MAN UNITED
Mazungumzo: Ryan Giggs (pichani akiwa na mke wake Stacey mjini Manchester) alikuwa Uholanzi kukutana na Louis van Gaal.
RYAN
Giggs leo mchana alikuwa nchini Uholanzi kwa ajili ya kufanya
mazungumzo na kocha mtarajiwa wa Manchester United, Louis van Gaal. Kocha huyo wa muda wa Man United alitakiwa kukutana na Mholanzi
huyo mjini Noordwijk, karibu na Hoteli ambayo timu ya Uholanzi inafanya
mazoezi, na wawili hao walitakiwa kukutana ili kujadili hatima ya
baadaye ya Man United. Giggs mwenye miaka 40 alionekana akitoka katika hoteli ya Van
Oranje mchana wa leo. Mkurugenzi mkuu wa Man United, Ed Woodward
alitakiwa pia kuwepo katika kikao hicho.
Giggs alitakiwa kukutana na Van Gaal kujadili hatima yake ya baadaye katika klabu ya Man United
Sehemu ya mkutano: Hoteli ya Van Orange mjini, Noordwijk ndio sehemu ambayo Giggs alitakiwa kukutana na Van Gaal
Mtarajiwa: Van Gaal anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha wa Man United wiki hii.
No comments:
Post a Comment