Katibu
wa Michezo kutoka Kampuni ya Proin, Godlisten Anderson akitambulisha
viongozi wa kampuni ya Proin Promotions kwa waandishi wa habari wakati
wa Mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika leo katika Hoteli ya
Southern Sun. Kampuni ya Proin imetangaza kudhamini ligi ya mpira wa
miguu kwa Wanawake inayotarajiwa kuanza Mwezi wa Nane.
Rais
TFF, Mh Jamal Malinzi na Mwenyekiti wa makampuni ya Proin, Mh Johnson
Lukaza wakitia saini katika mkataba wa makubaliano ya udhamini wa ligi
ya mpira wa miguu kwa wanawake itakayoanza mwezi wa Nane.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh6NCaDrIxFRm4BFXisnDAr09n_zTrMq-WjiWbsUv5KQSfAsmQth0-VslhjaW2HiaZwS9hJL1Q_eitGDGK8qPGbtpAtbA1LtVl9Cg67BjLyUrKKOTYf7KzPKmoN7n7JtVs0LigLVevkA3o/s1600/IMG_1518.JPG)
Raisi
wa TFF, Mh Jamal Malinzi (kushoto) akibadilishana mkataba wa udhamini
na Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza (katikati) mara
baada ya kumaliza kutiliana saini katika mikataba hiyo mbele ya
waandishi wa habari leo katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya
Southern Sun.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mpira Cha Wanawake, Bi Lina Muhando akiongea na Waandishi
wa habari waliohudhuria katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya
Sourthen Sun wakati Kampuni ya Proin ilitangaza kudhamini ligi ya
wanawake inayotarajiwa kuanza Mwezi wa Nane
Mwenyekiti
wa Makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza akijibu maswali ya waandishi
wa habari leo katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika
Hotel ya Southern Sun.
Rais
wa TFF, Mh Jamal Malinzi akiteta jambo na Mwenyekiti wa Makampuni ya
Proin Mh Johnson Lukaza wakati wa mkutano na waandishi wa habari
uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam.
Mwandishi
wa Habari kutoka gazeti la Jambo leo, Bi Asha Kigundula akiulizwa swali
katika mkutano huo.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Na Josephat Lukaza – Dar Es Salaam
Kampuni
ya Proin Promotions leo imetangaza rasmi kudhamini ligi ya mpira wa
miguu kwa wanawake inayotarajiwa kuchezwa mnamo mwezi wa nane mwaka huu
Jijini Dar Es Salaam ambapo itahusisha timu za wanawake washindi kutoka
mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Proin
Promotions imeingia mkataba wa miaka miwili kwaajili ya kudhamini ligi
hiyo. Proin Promotions inaendelea na lengo lake la kusaka vipaji katika
Mpira wa miguu kwa wanawake ambapo sasa Proin imeanza kusaka vipaji
katika Tasnia ya Filamu nchini kwa kuanzisha shindano liitwalo Tanzania
Movie Talents.
Akiongea
na Waandishi wa Habari leo Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Mh Johnson
Lukaza amesema Kuwa Sasa imefika wakati Kuanza kuibua vipaji vya mpira
wa miguu kwa wanawake ambapo ndio lengo kubwa la Kampuni yake hiyo ya
Proin Promotions. Vilevile aliongezea Kampuni yake tayari imeshaanza
mchakato wa kuibua vipaji vya Kuigiza kwa Kuanzisha Shindano
lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents ambapo kuanzia tarehe 17 Mwezi
huu kipindi cha kwanza kitaanza kurushwa hewani katika kituo cha Runinga
cha ITV kuanzia Mida ya Saa Nne Usiku na sasa ni zamu ya Watoto wa kike
kung’ara katika Mpira wa Miguu.
Vilevile
Kampuni ya Proin Promotions Imesema inawakaribisha makampuni mengine
pia kujitokeza kudhamini ligi hii ya mpira wa miguu kwa wanawake ambapo
itasaidia kuibu vipaji na kuifanya timu ya taifa ya wanawake ya Twiga
Stars kupata wachezaji wenye viwango vya juu ambao wataliletea Taifa la
Tanzania sifa na wao pia kuweza kuuzika kimataifa.
No comments:
Post a Comment