KOCHA
mpya wa Manchester United, Louis van Gaal amewaondoa Cesc Fabregas na
Toni Kroos katika orodha ya wachezaji anaotaka kuwasajii msimu ujao na
kuelekeza nguvu zake kwa wachezaji wengine akiwemo mpachika mabao wa Bayern Munich, Bastian Schweinsteiger.
Mholanzi
huyo amesema kwamba, ana matumaini kocha wa Munich, Pep Guardiola
atakuwa tayari kusikiliza ofa ya Pauni Milioni 10 kwa ajili ya kiungo
huyo mwenye umri wa miaka 29.
Schweinsteiger, ambaye jina
lake lilitajwa pia wakati wa David Moyes akiwa kazini United, pia ana
nia ya kwenda kukabiliana na changamoto mpya.

Anamuhitaji: Bastian Schweinsteiger anaweza kupatikana kwa dau la Pauni Milioni 10 na Van Gaal anamuhitaji kiungo huyo
Pia
Van Gaal anawataka beki wa kulia wa Feyenoord, Daryl Janmaat, beki wa
kati Bruno Martins Indi na beki wa Ajax, Daley Blind na mpango wa
kumsajili Kevin Strootman wa AS Roma bado upo, mara itakapothibitika anaweza kupona maumivu yake goti.
Wakati
huo huo, Danny Welbeck amesema amevurugwa kwa kukosa nafasi katika
kikosi cha kwanza cha United msimu uliopita, kwani mshambuliaji huyo wa England anataka kupangwa katikati athibitishe uwezo wake wa kufunga kwa kiwango cha juu katika klabu na timu ya taifa.
Welbeck
amefunga mabao manane katika mechi 21 za timu ya taifa, lakini alikuwa
akisotea namba kikosi cha kwanza chini ya David Moyes United.
No comments:
Post a Comment