Ni miaka mingi sasa imepita toka ifahamike kuwa CEO wa MJ Records
Joachim Kimaryo aka Master J na mwimbaji Sarah Kaisi aka Shaa ni
wapenzi, kiasi mpaka sasa hata wanapoulizwa kwenye interviews na
mitandao ya kijamii hukiri kuwa wao ni couple.
Lakini mama mzazi wa Master J ameona kuna haja ya mwanae kuuweka wazi
rasmi uhusiano wao ili jamii iwe na taarifa sahihi, hivyo amemshauri
mwanaye kuwaita waandishi wa habari kuzungumzia uhusiano wao na mipango
yao ya ‘ndoa’.
“Hili ni jambo ambalo kusema kweli limekuwa kubwa sana sasa hivi,”
Alisema MJ kupitia E-News ya EATV. “Nilikuwa nimekaa na mama yangu mzazi
amenishauri ameniambia sikiliza uite watu wa media wewe na huyo Sarah
muwe open kwa sababu kiukweli mnavyoendelea kukaa kimya kila mtu anakuwa
ana assume mambo yake ambayo mwisho wa siku yanaweza kuleta madhara
flani”.
Mj ambaye ni baba wa watoto watatu ameahidi kuwaita waandishi wa habari
mwaka huu ili kumtambulisha rasmi Shaa kama mpenzi wake na mipango yao
ya baadaye.
No comments:
Post a Comment