Sunday, 13 April 2014

REAL MADRID YAREJEA KILELENI LA LIGA

Madrid imehitimisha wiki nzuri kwa kurudi
kileleni mwa La Liga, baada ya usiku wa jana
kuitandika Almeria mabao 4-0, ikitoka kutinga
Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ikicheza bila mwanasoka bora wa dunia,
Cristiano Ronaldo, Real ilipata mabao yake
kupitia kwa Angel Di Maria dakika ya 28, Gareth
Bale dakika ya 53, Isco dakika ya 56 na Morata
dakika ya 85.
Real sasa inatimiza pointi 79 za mechi 33 na
kupaa kileleni kwa wastani wa mabao kwa kuwa
na pointi sawa na Atletico Madrid, ikiizidi kwa
pointi moja Barcelona. Lakini Real wanaweza
kushuka hadi nafasi ya pili leo iwapo Atletico
Madrid itaifunga Getafe.
Katikati ya wiki, Real imeitoa Borussia Dortmund
katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na kutinga Robo
Fainali, ambako itakutana na mabingwa watetezi,
Bayern Munich.

No comments:

Post a Comment