Jumamosi iliyopita matangazo ya Television ya
taifa yalikatika wakati ikiwa live kwenye bunge la
katiba ambapo Mh. Tundu Lissu alikua
akiwasilisha maoni ya wachache ambako
kulisababisha Mwenyekiti kuahirisha bunge hilo
mara moja baada ya kugundulika hawakuwa
wanaonekana live.
Kukatika huko kwa matangazo ambako badae
kulitangazwa kwamba ni kutokana na hali ya
hewa kulifanya TBC itupiwe lawama au
malalamiko yakiwemo kutoka kwa baadhi ya
viongozi na Wananchi huku baraza la habari
likisema ni kitendo cha aibu na watafatilia kujua
kama ni kweli hali ya hewa au hujuma.
Baada ya hayo yote na kauli zilizotolewa na
Wanasiasa mbalimbali baadae, Samwel Sitta
ambae ni Mwenyekiti wa bunge la katiba hapa
Dodoma ametoa taarifa rasmi akisema >>
‘kuanzia sasa matangazo ya live bungeni TBC1
yakikatika hatutawezi kukatisha kuendelea na
bunge’
‘Tunazingatia kwamba ipo Radio na Wananchi
wengi wa Tanzania wanasikiliza radio na mtu
mwenye TV hawezi kushindwa kununua radio
kwa hiyo hatuwezi kukatiza kila wakati, ikiwa
radio inaendelea kazi yetu humu ndani
itaendelea’ – Samwel Sitta
Tuesday, 15 April 2014
SITTA"KUANZIA SASA TBC1 WAKIKATA MATANGAZO HATUWEZI KUKATISHA KUENDELEA NA BUNGE"
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment