Amekua mmiliki wa vichwa vya habari
kutokana na ripoti mbalimbali ambazo zimekua
zikimnukuu kwa kudai kutozitaka serikali mbili
lakini leo April 15 2014 amezungumza kwenye
maonyesho ya miaka 50 ya muungano ya
kuzitoa hizi kauli zifuatazo.
1. ‘Pamoja na milima na mabonde, muungano
huu umedumu miaka 50, nchi nyingine
zilishindwa, l azima tufanye tathmini hasa ya
muungano wetu, lazima vijana waelimishwe vp
muungano uliundwa, tulianzia vipi’
2.‘Ukitaka upate maenedeleo, yatambue
mafanikio yako lakini pia usisahau matatizo
yako, ni ni moja.. kufanya vizuri, Sidhani katika
Tanzania kama kuna watu hawataki muungano,
na kama wapo ni wachache, muungano
uendelee ndio la msingi’
3. ‘ Sio dhambi watu kuwa na fikra tofauti, sio
dhambi hata kidogo kwa sababu hatuwezi wote
kuwa na fikra aina moja, Wanaotaka serikali
moja wasibezwe, mbili wasibezwe, wanaotaka
tatu na serikali ya mkataba wasikilizwe pia’
4. ‘ Wako wanaoamini kwamba matatizo ya
muungano yako kwenye muundo, tuwasikilize
wana hoja gani, Mwaka 1963 Malaysia na
Tanganyika maendeleo ya sehemu zote hizi
yalikua sawa, mwaka 2014 tujiulize,
c hangamoto kwetu ni vipi tutakua na
muungano utakaokua ni chachu ya maendeleo
ya haraka, mambo ya 74 ni tofauti na 2014′
5. ‘Tuwe makini sana, sote ni wa nchi moja,
tujiepushe na kikundi chochote kuona wao
wana haki zaidi, Watanzania wote sawa,
w ajumbe wa bunge maalum waangalie maslahi
ya nchi, muungano huu ni wa nchi 2 zilizokua
dola huru na kuungana kwa hiari’
6. ‘ Tupate katiba ambayo itaondoa migogoro,
kero iwe ni historia… hili swala lisiwepo tena,
t usiende kwenye maamuzi ya harahaharaka
tukasema serikali mbili au tatu bila kuangalia
athari zake, k atiba ya Znz inasema ni miongoni
mwa nchi mbili za muungano, ya Muungano
inasema Tz ni nchi moja, huo ni mgogoro’
7. ‘ Nadhani Warioba walivyopendekezwa
waliona hisia za Znz zilivyo, tunataka katiba
itakayotambua usawa wa nchi mbili, h akuwezi
kuwa na katiba ambayo itamridhisha kila mtu
lakini angalau wengi wao waridhike’
Tuesday, 15 April 2014
SEIF SHARIFF HAMAD KAZUNGUMZA LEO, KAULI ZAKE 7 KUHUSU MUUNGANO ZIKO HAPA...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment