NYOTA
Cristiano Ronaldo amempoteza Lionel Messi kwa mara nyingine tena, baada
ya usiku wa jana kuvunja rekodi ya mabao ya Muargentina huyo, na
kuibuka mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwa msimu mmoja wa Ligi ya
mabingwa Ulaya.
Mkali
huyo wa Ureno jana alifunga mabao mawili katika ushindi wa wa Real wa
4-0 kwenye mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali dhidi ya Bayern Munich,
na kufikisha jumla ya mabao 16 kwa msimu huu.
Rekodi hiyo ya Ronaldo inaipiku rekodi ya Lionel Messi - ambaye alifunga mabao 14 kwa Barcelona msimu wa 2011-12.
Tangu ahamie Madrid mwaka 2009, mshambuliaji huyo amefunga jumla ya mabao 250 katika mechi 243 za klabu hiyo.
Mwanasoka
huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 29, kufunga mabao
mawili haikuwa rekodi pekee jana aliyoweka mjini Munich.
Mabao
mawili ya mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d'Or pia yanamfanya awe
mchezaji wa tatu katika historia ya mashindano hayo kufikisha mabao 50
au zaidi aliyoifungia timu moja katika Ligi ya Mabingwa.
Ronaldo
aliyefunga mabao 51 katika mechi 50, anamfuataia gwiji wa Real, Raul
MABAO 16 YA RONALDO MSIMU HUU
Mabao
mawili ya Cristiano Ronaldo aliyoifungia Real Madrid dhidi ya Bayern
Munich wa jana yanamfanya atimize mabao 16 msimu huu katika Ligi ya
Mabingwa.
Anakuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwa msimu mmoja wa Ligi ya Mabingwa Ulaya...
Galatasaray 1-6 Real Madrid, Septemba 17, 2013 - Ronaldo mabao matatu (3)
Juventus 2-2 Real Madrid, Novemba 5, 2013 - Ronaldo bao moja (1)
Schalke 1-6 Real Madrid, Februari 26, 2014 - Ronaldo mabao mawili (2)
Real Madrid 3-1 Schalke, Machi 23, 2014 - Ronaldo mabao mawili (2)
Real Madrid 3-0 Borussia Dortmund, Aprili 2, 2014 - Ronaldo bao moja (1)
Bayern Munich 0-4 Real Madrid, Aprili 29, 2014 - Ronaldo mabao mawili (2)
No comments:
Post a Comment