Jaji wa mahakama nchini Misri, amewahukumu
kifo watu 683 akiwemo kiongozi wa kundi la
Muslim Brotherhood Mohammed Badie.
Mawakili wa watuhumiwa wanasema kuwa
wateja wao walikabiliwa na makosa mengi
yakiwemo, kushambulia kituo cha polisi mjini
Minya mwaka 2013 ambapo polisi mmoja
aliuawa.
Jaji huyo pia alibatilisha hukumu ya kifo
iliyotolewa kwa watu 492 kati ya watu 529.
Hukumu hiyo ilipitishwa mwezi Machi na sasa
watahudumia kifungo cha maisha jela.
Kesi na kasi ya kuzisikilizwa kwa kasi hizo,
imesababisha hasira na kukosolewa na shirika la
kutetea haki za binadamu la Umoja wa Matifa
UN.
Kadhalika shirika la Huma Rights Watch
limelalamika kuwa kesi hizo zilisikilizwa tu kwa
saa chache huku mahakama ikiwazuia mawakili
kuwawakilisha washitakiwa.
Duru zinasema kuwa jamaa wa watuhumiwa
waliokuwa wanasubiri nje ya mahakama walizirai
baada ya kupokea taarifa za hukumu hiyo.
Mwezi jana shirika la kutetea haki za binadamu la
Umoja wa Mataifa, lililaani kesi hizo likisema
kuwa zinakiuka sheria ya kimataifa ya haki za
binadamu.
Msemaji wa shirika hilo, Navi Pillay, alisema kuwa
kesi hiyo ilikumbwa na makosa mengi ya
utarataibu.
Maafisa wa utawala nchini Misri wamekuwa
wakiwasaka na kuwakamata wapiganaji wa
kiisilamu na wanachama wa vuguvugu la Muslim
Brotherhood ambao walimuingiza mamlakani
aliyekuwa Rais Mohammed Morsi ambaye
baadaye aliondolewa na Julai.
Mamia wameuawa huku maelfu ya raia
wakikamatwa.
Monday, 28 April 2014
WATU 683 WAHUKUMIWA KIFO MISRI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment