Wednesday, 4 June 2014

BRAZIL NA NEYMAR WATOA ONYO KOMBE LA DUNIA...WAIFUMUA PANAMA 4-0

WENYEJI wa Fainali za Kombe la Dunia, Brazil wametoa onyo- baada ya kuifumua Panama mabao 4-0 katika mchezo wa kirafiki usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Serra Dourada mjini Goiania.
Neymar ameanza kuipoa ishara dunia kwamba atatisha katika fainali hizi kwa kufunga bao tamu la mpira wa adhabu dakika ya 27.
Kabla ya mapumziko, Brazil ikapata bao la pili kupitia kwa mchezaji mwenzake Neymar pale Barcelona, Dani Alves aliyefunga dakika ya 40.
Kipindi cha pili kilipoanza tu, Hulk akawainua tena vitini Wabrazil kwa kufunga bao la tatu dakika ya 46 kabla ya Willian kunaliza kazi dakika ya 73 na kuhitimisha ushindi wa 4-0.
Kikosi cha Brazil kilikuwa: Cesar, Dani Alves/Maicon, dk46, Luiz/Henrique, dk70, Dante, Marcelo/Maxwell, dk46, Ramires/Hernanes, dk46, Gustavo, Oscar/Willian, dk63, Fred/Jo, dk61, Neymar na Hulk.
Panama: McFarlane/Calderon, dk58, Machado/Jimenez, dk56, Carroll/Rodriguez, dk67, R Torres/Cummings, dk59, Gomez, Quintero, Cooper/Torres, dk56, Henriquez, Munoz na Tejada/Nurse, dk46.
Nyota wa Samba: Neymar akishangilia baada ya kuofungia Brazil bao la kwanza katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Panama mjini Goiania 
Pick that one out! Neymar curled a free-kick into the top corner to set Brazil on their way to victory
Kitu hicho! Neymar akipiga mpira wa adhabu uliozaa bao la kwanza la Brazil
Powerless: Panama goalkeeper Oscar McFarlane was at full stretch but was unable to deny Neymar's strike
Kipa wa Panama, Oscar McFarlane akidaka hews baada ya shut la mpira wa adhabu wa neymar kumpita na kiting nyavuni

No comments:

Post a Comment