Monday, 9 June 2014

JENNIFER LOPEZ AJITOA SHEREHE ZA UFUNGUZI KOMBE LA DUNIA, FIFA YATHIBITISHA HATAIMBA ALHAMISI

Kwenye kipaza: Jennifer Lopez amejitoa kwenye sherehe za ufunguzi wa Kombe la Dunia
 MWANAMUZIKI Jennifer Lopez hataimba limbo maalum wa Kombe la Dunia sambamba na wasanii wenzake nyota, Pitbull na Claudia Leitte katika sherehe za ufunguzi wa michuano hiyo Brazil, taarifa ya FIFA imesema jana.
Bodi hiyo ya soka duniani imesema Lopez hataimba Alhamisi wiki hii kama ilivyopangwa awali kutokana na sababu za kitaalamu ambazo hazikutajwa.
Wawakilishi wa mwimbaji huyo hawajasema sababu ya Lopez kutoweza kuungana na wenzake. 

No comments:

Post a Comment