Sunday, 15 June 2014

MESSI AING'ARISHA ARGENTINA IKIUA 2-1 KWA MBINDE KOMBE LA DUNIA

ARGENTINA imeanza vyema Kombe la Dunia
baada ya usiku huu kuilaza Bosnia-Herzegovina
mabao 2-1 katika mchezo wa Kundi Kombe la
Dunia Uwanja wa Maracana mjini Rio de
Janeiro, Brazil.
Shukrani kwake Mwanasoka bora wa zamani wa
dunia, mshambuliaji wa Barcelona ya Hispania,
Lionel Messi aliyefunga bao la pili la Argentina
dakika ya 65 akimalizia pasi ya Gonzalo Higuain.
Sead Kolasinac aijifunga dakika ya tatu katika
harakati za kuokoa kuipatia Argentina bao la
kwanza kabla ya Vedad Ibisevic kutumia pasi ya
Senad Lulic kuisawazishia Bosnia dakika ya 84.
Kikosi cha Argentina kilikuwa; Romero,
Campagnaro/Gago dk45, Fernandez, Garay,
Zabaleta, Maxi Rodriguez/Higuain dk45,
Mascherano, Di Maria, Rojo, Messi na Aguero/
Biglia dk86.
Bosnia-Herzegovina; Begovic, Mujdza/Ibisevic
dk70, Bicakcic, Spahic, Kolasinac, Besic,
Hajrovic/Visca dk72, Pjanic, Misimovic/
Medunjanin dk74, Lulic na Dzeko.

No comments:

Post a Comment